millard ayo ( @millardayo ) Instagram Profile

millardayo

millard ayo

East African Radio Personality |
CloudsFM |
Bookings: millard@millardayo.com | @ayotv_
📍 🇹🇿 🇺🇸 🇰🇪 🇷🇼

 • 33.9k posts
 • 6.2m followers
 • 1.7k following

millard ayo Profile Information

 • Simba wamemtangaza Sven Vanderbroeck (40), Raia wa Ubelgiji kama kocha wao Mkuu, Sven alikuwa Kocha Msaidizi wa Cameroon iliyotwaa AFCON 2017, Gabon na amewahi kuwa Kocha Mkuu wa Zambia 2018/2019, Simba haijaweka wazi imeingia mkataba wa muda gani na Sven. #MillardAyoSPORTS

 •  1,417  42  11 December, 2019
 • Shop with us on this holiday season. @gsmmall

 •  269  0  11 December, 2019
 • Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema kitendo cha Mussa Msola 'Hitler' kuachiwa kwa Msamaha wa Rais Jana kisha alipotoka akaenda kuvunja Gesti kwa dhamira ya kuiba kinaashiria Maisha yake yeye ameamua yawe Gerezani na kusema wao hawana budi kumpeleka Gerezani tena.
_
"Ni masaa nane tu baada ya kuachiwa Mtuhumiwa huyu aliyekuwa huru ilipofika majira ya saa tisa usiku,alijikuta ameshawishika kwenda kufanya tukio la uvunjaji wa Gesti, yupo kituo cha Polisi na tunapomhoji yeye anakubaliana na hii kesi kuwa kweli ni tamaa zilimshika na akaenda kufanya uvunjaji, tutampeleka Mahakamani na atarudi tena Gerezani"- RPC NJOMBE
Full Video ipo YouTube ya 'Millardayo'
(📹 via @ayotv_)

 •  5,997  365  11 December, 2019
 • Ikiwa imepita siku moja tu tangu yeye na wenzake waachiwe Mkoani Njombe kwa msamaha wa Rais Magufuli, Kijana Mussa Msola maarufu kwa jina la Hitler, amekamatwa tena na kurudishwa mahabusu kwa tuhuma za kuvunja nyumba moja ya kulala wageni Mjini Makambako akidhamiria kuiba.
#MillardAyoUPDATES

 •  11,752  765  11 December, 2019
 • Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu aliyekuwa Rais wa TFF Jamali Malinzi na Katibu wake, Selestine Mwesigwa kulipa faini ya Shilingi Laki Tano ama kwenda jela miaka miwili, baada ya kukutwa na kosa la kughushi nyaraka.
_
Mahakama hiyo imemuachia huru Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Karani wa TFF, Flora Rauya kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao.
_
Hukumu ya Malinzi na wenzake ambao wamesota Gerezani kwa miaka miwili na nusu imechukua takribani saa 5 ambapo ilianza kusomwa saa 8:30 mchana hadi saa 12 jioni.
_
Hata hivyo Malinzi na Mwesigwa wamerudishwa Gerezani kwasababu ya kushindwa kulipa faini hiyo kwa siku ya leo, ambapo kesho Desemba 12, 2019 wanatarajia kulipa faini hiyo ili waachiwe huru.

 •  3,903  243  11 December, 2019
 • Asanteni @fgamwema kwa kunialika kwenye mahafali ya 3 !!! amazing academy, beautiful kids kiukweli!! 👌🏿

 •  10,614  105  11 December, 2019
 • Kufuatia kushika kasi kwa vitendo vya Wazazi na Walezi kuwapeleka Mabinti zao wenye umri wa kati ya miaka 10 hadi 15 kwa Waganga wa kienyeji ili kuogeshwa Dawa ya kuwavutia Wanaume inayoitwa 'SAMBA', Serikali imeombwa kupiga marufuku vitendo hivyo kwakuwa vinachochea maambukizi ya virusi vya ukimwi na mimba za utotoni.
_
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ‘Kivulini’ linalojihusisha na kupinga ukatili wa kijinsia Yassin Ally amesema vitendo hivyo vinafanyika kwa wingi sana Wilaya ya Kishapu na maeneo mengine ya Mkoa wa Shinyanga.
_
"Nimefika Shinyanga baadhi ya Shule Wanafunzi ni watoro nilipodadisi niliambiwa wanaenda kuogeshwa dawa za mvuto kwa Wanaume (SAMBA)-Yassin
_
"Viongozi wapige marufuku Mila hizi potofu na waganga wa jadi wanaotafuta kipato kwa mtindo huu wa kudanganya Watu wadhibitiwe, haiwezekani ukamvuta Mwanaume kwa Dawa ili ampende Binti, waacheni Mabinti wakifika umri watachagua wanaowapenda"- Yassin

 •  5,228  187  11 December, 2019
 • Club ya Yanga SC imetangaza rasmi kuvunja mkataba na mchezaji wake Juma Balinya kutoka Uganda, inadaiwa kuwa mkataba huo umevunjwa kwa makubaliano ya pande mbili wakati huu kukiwa na madai ya mishahara #MillardAyoSPORTS

 •  5,789  125  11 December, 2019
 • Hatima ya Vigogo wa TFF akiwemo aliyekuwa Rais wake, Jamal Malinzi na wenzake inajulikana leo December 11, 2019 ambapo muda huu Washtakiwa wapo ndani ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu tayari kwa kusubiri hukumu yao katika kesi inayowakabili ya utakatishaji fedha.
_
Washitakiwa hao ambao wako rumande kwa zaidi ya miaka miwili, hukumu yao iliahirishwa kwa mara tatu mfululizo, kwa mara ya kwanza hukumu ilipangwa October 25 mwaka huu ikashindikana kwasababu Hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi Maira Kasonde alihamishwa kituo cha kazi.
_
Novemba 7, 2019 Mahakama hiyo pia ilishindwa kusoma hukumu kwa sababu Hakimu Kasonde licha ya kuhamishwa Kituo cha kazi pia hakuwa amemaliza kuandika hukumu hiyo na ikapangwa December 5, 2019 napo ikashindikana.

 •  1,634  30  11 December, 2019
 • Leo December 11, 2019 nakusogezea story PART 2 ya Mariam Obret @maryam36k ambaye alipata ajali December 04, 2011 iliyompa tatizo la uti wa mgongo ambapo kwa sasa hawezi kutembea na anatumia wheelchair.
_
Leo Mariam anatuelezea maisha yake ya uhusiano wa kimapenzi ambapo anasema "Kwa sasa siko kwenye uhusiano ila nilipopata tatizo niliingia kwenye uhusiano, Boyfriend wa kwanza aliniacha kwasababu nilipata tatizo" - Mariam
_
"Boyfriend wa pili ni matatizo ya kawaida tu yalitokea tukaachana, Boyfriend wa kwanza alianza kunichunia Christmas na Mwaka mpya kisha Boxing day akaniacha rasmi"- Mariam
Full Video ipo YouTube ya ‘millardayo’
Cc: @pascal_tza

 •  10,935  320  11 December, 2019
 • Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe anataka Wananchi wa Handeni wapate majibu na kutatua ishu zao kabla mwaka haujaisha.
_
Gondwe ambae amejizolea sifa nyingi za kuipambania Handeni ikiwemo za ujenzi wa Shule, ameleta suluhisho kupitia kitu kinaitwa ONE STOP JAWABU ambapo Wakazi wa Handeni watatatuliwa ishu zao papohapo kwa wiki hii nzima.
_
‘Tunamshukuru sana Mkuu wa Wilaya kwa kuandaa zoezi hili ambalo limekusanya Wananchi wote wa Handeni kuja na kero zao hasa wale ambapo hawajapata namba za NIDA”
_
Kwenda mbali zaidi DC Gondwe @ggondwe amewaleta pia Mawakili kutoka Chama cha Mawakili kuwepo eneo la tukio wiki nzima ili kuwahudumia Wananchi kwenye mahitaji yao ya kisheria na migogoro ya ardhi.

 •  1,124  16  11 December, 2019
 • Shop with us on this holiday season. @gsmmall
 • Shop with us on this holiday season. @gsmmall

 •  1,010  0  11 December, 2019